Mukoko, Yacouba waitwa Burkina Faso, DR Congo

0
389

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Nyota wawili wa Yanga, Mukoko Tonombe na Songne Yacouba wameteuliwa katika vikosi vya timu za taifa za DR Congo na Burkina Faso vinavyojiandaa na mechi za kimataifa za kirafiki mwezi ujao.

Kocha mpya wa DR Congo, Hector Cuper amemjumuisha kiungo Mukoko Tonombe katika kikosi chake kinachojiandaa na mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Tunisia na Cape Verde.

mukokoooopic

Songne Yacouba

Kikosi hicho cha DR Congo kimejaza idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya bara la Afrika

Wakati Tonombe akijumuishwa katika kikosi cha DR Congo, nyota mwingine wa Yanga, Songne Yacouba naye ameteuliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso ambacho kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ivory Coast