Wednesday, August 4, 2021

Mtoto wa rais Mali matatani kuhusu kutoweka kwa mwandishi

Bamako, Mali (AFP). Shirika la Interpol limetoa hati ya kimataifa ya kumkamata Karim Keita, mtoto wa rais wa zamani wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, akihusishwa na tukio la mwaka 2016 la kutoweka kwa mwandishi wa habari za uchunguzi, watu walio katika duru za sheria wamesema.

Hati hiyo ya mumkamata Keita, ambaye pia alikuwa mwanasheria mwenye ushawishi, ilitolewa baada ya kuombwa na mahakama jijini Bamako, wamesema watu hao waliotaka wasitajwe majina.

Habari za hati ya kukamatwa ilithibitishwa pia na mtu aliye ndani ya ofisi ya shirika hilo la kimataifa la polisi la Interpol na ambaye pia aliomba asitajwe jina.

Keita amekuwa akiishi jijini Abidjan, Ivory Coast, tangu kutokea mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa baba yake madarakani Agosti mwaka 2020.

Birama Toure, mwandishi wa habari za uchunguzi, alikuwa akifanya kazi gazeti la kila wiki la Le Sphinx miezi kadhaa kabla ya kutoweka kwake.

Hajaonekana tangu Januari 29, 2016, kw amujibu wa familia yake na mkurugenzi wa jarida hilo, Adama Drame.
Drame alisema Toure alikuwa akifanyia kazi habari ambaye ingeshusha hadhi ya Keita na aliwasiliana aye kuhusu habari hiyo kabla hajatoweka.

Advertisement

Drame na familia ya Toure wanatuhumu kwamba alitekwa, kuteswa na kuuawa baada ya kukaa kizuizini kwa miezi kadhaa.

Keita amekuwa akikanusha kuhusika na tukio hilo na mwaka 2019 alifungua kesi ya madai dhidi ya mkurugenzi wa jarida hilo na mwandishi wa redio, akidai kudhalilishwa.

Mahakama ya Mali ilitupilia mbali kesi hiyo kwa sababu za kiufundi, lakini Drame, akihofia usalama wake, alikimbilia nchini Ufaransa

Related Posts

Comments

Stay Connected

22,044FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe

Recent Stories