Sunday, August 1, 2021

Mpango mpya wa kodi na uwekezaji wa makaazi Zanzibar unatarajiwa kufungua fursa kubwa za kimataifa

MAZIZINI, / AGILITYPR.NEWS / July 07, 2021 / Tangazo kwa Umma

Mpango mpya wa kodi na uwekezaji wa makaazi Zanzibar unatarajiwa kufungua fursa kubwa za kimataifa

Serikali imechukua hatua muhimu ya kuifanya Zanzibar kuwa kivutio kwa wawekezaji wa kigeni wanaotaka kuwekeza barani Afrika

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuwa Zanzibar, mojawapo ya kivutio kikubwa cha safari zakitalii a barani Afrika, sasa ina mpango mpya wa kodi na ukaazi kwa wageni unaowawezesha kuishi na kuwekeza katika kisiwa hiki.

Hatua hii inayoleta mabadiliko makubwa imekuja kufuatia mipango muhimu wa kuimarisha miundombinu na ikukuza utalii rafiki ambayo iliwezesha Tanzania kuwa kuwa kivutio cha utalii kinachoweza kukabiliana na changamoto kubwa iliyoletwa na janga la Covid-19 mnamo mwaka 2020.

Hadi sasa, Sheria ya Uwekezaji ya 2018 ilitoa taratibu na vigezo vya kupatiwa Hadhi ya kuwa Mwekezaji Mkakati (Strategic Investment Status-SIS) inayotoa fursa na vivutio kwa wawekezaji walioidhinishwa , lakini haikutoa fursa hizo kwa wale wanaotaka kununua mali nchini..

Matokeo yake ni kwamba Zanzibar haikuweza kuvutia wawekezaji wakubwa walioidhinishwa kwa ajili ya uwekezaji unaozalisha , ambapo nchi kama Mauritania , Dubai, Omani, Singapuri na nchi nyinginezo zimestawi sana baada ya kutekeleza mkakati huu.

Kwa uanzishwaji wa mpango huu mpya wa wawekezaji, uliotangazwa na Serikali siku ya Jumanne, wanunuzi wa kigeni sasa watapewa fursa ya kujiongezea faida nyingi, na hivyo kuvutia wawekezaji na kuinua uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Wawekezaji walioidhinishwa wa mali zisizohamishikasasa wanaweza kupewa kibali cha ukaazi kama wawekezaji, kwa maana hiyo wataruhusiwa kuishi Zanzibar kama raia wa kigeni. Pia hawatoruhusiwa kuishi Zanzibar daima.

Kodi mpya na faida za ukaazi kwa wawekezaji i wa mali isiyohamishika:

1)     Kodi ya mapato haitatozwa kwa kipato na mali ya jumla

2)     Kibali cha ukaazi kitatolewa kwa wanunuzi wa nyumba (VILLA) pamoja na mwenza wake na watoto wa umri wa chini ya miaka 20 wasiozidi 4

3)     Mnunuzi wa kwanza atalipa asilimia 50 tu ya faida ya kawaida ya mtaji kwa uuzaji wa nyumba moja, atalipa kwa asilimia 5badala ya asilimia 10

4)     Wageni wanaruhusiwa kumiliki mali

5)     Usajili wa umiliki utafanywa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) (ZIPA)

6)     Hakuna Kodi ya ongezeko la thamani (VAT)utakaotozwa kwa kukodisha au kuuza nyumba

7)     Kodi ya mapato itatozwa kwa kiwango nusu kwa kipato cha ndani i tu, asilimia 15itatozwa badala ya asilimia 30 (hii inawahusu wageni tu )

8)     Wawekezaji wanaruhusiwa kutuma faida nje baada ya kulipa kodi

9)     Kibali cha makazi kinatumika kwa muda tu plae ambapo mnunuzi anamiliki mali husika (kibali kinaweza kuchukuliwa upya kila baada ya miaka miwili kwa ada ya Dola za kimarekani 3050 kwa mwekezaji mkuu na dola za kimarekani 550 kwa kila mtegemezi wake)

10) Kibali cha kufanya kazi hakitolewi, lakini mwajiri anaweza kukiomba kwa njia nyengine

11) Hakuna kiwango cha chini zaidi kinachohitajika ili mwekezaji aombe madai ya faida

Wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika biashara kama vile mikahawa, vilabu vya kuuza pombe, michezo ya majini na shughuli za rejareja watapata faida sawa na wawekezaji wa kuuza, kununua majengo na ardhi na upangishaji wa nyumba (real estate investors) kupitia miradi iliyoidhinishwa ya “Uwekezaji mkakati ” tu (yaani uwekezaji ambao mwekezaji aliyeidhinishwa ametimiza vigezo vilivyo ainishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ukuzaji na Kulinda Vitega Uchumi Zanzibar)

Kodi mpya na faida za ukaazi kwa wawekezaji wa biashara tu:

1)     Wageni wanaruhusiwa kumiliki mali

2)     Hakuna ada ya leseni ya biashara kwa miezi mitatu ya kwanza

3)     Kodi ya kampuni: Kodi ya kipato ni bure na haitatozwa kwa miaka mitano (5) ya kwanza. Baada ya miaka mitano (5) ya kwanza: asilimia hamsini (50)itatozwa (Kodi ya mapato itakuwa ni asilimia thelathini (30), kwa hivyo itakuwa ni asilimia kumi na tano (15) tu )

4)     Wawekezaji wanaweza kurudishiwa faida baada ya kulipa kodi

5)     Msamaha wa wa asilimia mia moja (100)100 kwa kodi ya zuio inalipwa benki za kigeni

6)     Punguzo la asilimia mia moja (100) ya kiwango cha gharama za uchakavu ndani ya miaka mitano(5)

7)     Kibali cha kazi na ukaazi kwa mwekezaji na wafanyakazi wake.

Pennyroyal Ltd ni mwekezaji wa muda mrefu, muanzilishi na meneja wa Blue Amber Zanzibar, na ni mradi wa kwanza wa uwekezaji mali zisizohamishika uliopewa hadhi ya kuwa Mwekezaji Mkakati (SIS) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Blue Amber ni biashara mseto ya hoteli za anasa, zilizo kwenye fukwe za bahari yenye ukubwa wa hekta 411 zilizopo Muyuni Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Zanzibar. Inashirikisha huduma za makazi, hoteli, utalii na huduma za jamii na umma

Hii ndiyo biashara ya pekee ya “Uwekezaji Mkakati i” inayohusisha mali zisizohamishika katika Zanzibar iliyo na pwani asili ambayo haijaharibiwa, inayotoa muonekano wa pwani safi ya Muyuni na Kisiwa cha Mnemba.

Ujenzi wa makazi ya kwanza ya majumba ya villa na kituo cha wageni ulianza katika robo ya kwanza ya 2020 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 hadi 24 ijayo. Awamu zinazofuata zitajumuisha ujenzi wa miradi mingine ya hoteli, makazi na biashara za rejareja karibu na majengo makuu.

Awamu ya 1 ya mradi hu inatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili ijayo:

Kufuatia kuanzishwa kwa mpango mpya wa uwekezaji wenye faida lukuki , wawekezaji wanatarajia kuwa wanunuzi kutoka nje ya nchi wanavutiwa zaidi, haswa ikizingatiwa kuwa mwaka jana Tanzania iliunga mkono mwendendo wa kimataifa wa kusafiri.

Nchi hii, haswa Zanzibar, ilishuhudia viwango vya juu vya wageni kinyume na iliyotarajiwa mwaka 2020, licha ya hali mbaya zilizosababishwa na janga la ugonjwa wa virusi vya korona 19 (UVIKO 19).

Tanzania ilirekodi zaidi ya watalii 620,000 wa kigeni kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 –karibu ya wagenilaki mbili (200,000) zaidi ya ilivyotarajiwa.

Utekelezaji wa haraka wa Taratibu za Kawaida za Uendeshaji zinazowataka wageni kuwasilisha vyeti vya ithibati wa hali yao ya UVIKO 19 , hatua ambazo pia zilitumika kwa wadau katika sekta ya utalii wa ndani, ambazo zilichangia sana kuleta mafanikio nchini.

Mikakati madhubuti iliyotekelezwa na serikali ilivutia Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani ambalo liliipa Tanzania ‘Stempu ya Usalama wa Kusafiri’ mwezi Agosti – hartua ambayo ni mafanikio makubwa ikizingatiwa hofu kubwa iliyotanda ulimwenguni kuhusiana na UVIKO 19

Kuanzia wakati huo, janga hilo lilifika katika ukanda wa Afrika, viongozi wa nchi hizi walichukua hatua madhubuti kukabliana nalo, wakiendelea na mipango ya kuifanya Tanzania kuvutia zaidi kwa wawekezaji wa kigeni.  

Mwezi Januari, Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Dr. Hussein Ali Mwinyi alitia saini Hati ya Maelewano (MoU) ya Ujenzi wa Bandari ya Mafuta wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 230 itakayokuwa Kaskazini mwa Unguja.

Mara baada ya kukamilika, mradi huu utajumuisha sehemu za kuweka kontena na mizigo mchanganyiko,baharini,bandari ya kuhudumia mafuta na gesi asilia na chelezo cha kukarabati meli .

Mnamo tarehe 30 Mei, , Kituo cha tatu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA), kitafunguliwa ili kuimarisha ubora wa huduma na ushughulikiaji wateja kwa wageni wa Kisiwa hiki.

Kuhusu Blue Amber Zanzibar:

Blue Amber ni biashara mseto ya hoteli za anasa, zilizo kwenye fukwe za bahari yenye ukubwa wa hekta 411 zilizopo Muyuni Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Zanzibar. Inashirikisha huduma za makazi, hoteli, utalii na huduma za jamii..

Blue Amber inajengwa na Pennyroyal Ltd na ni mradi wa kwanza wa mali isiyohamishika kupewa tuzo ya “Hadhi ya Uwekezaji Mkakati ” na Serikali ya Zanzibar.Hati hiyo inawapa fursa watu wasio raia kuwa wakaazi wa kudumu na kunufaika na kodi zinazovutia ikiwa watanunua mali ndani ya mradi ulio na “Hadhi ya Uwekezaji Mkakati

Mradi huu utatekelezwa kwa awamu kadhaa. Awamu ya kwanza ilihusisha kufyeka eneo la ujenzi, kujenga uzio wa mpaka, na kujenga miundombinu ya barabara. Ujenzi wa makazi ya kwanza ya nyumba (Villa) na kituo cha wageni ulianza katika robo ya kwanza ya 2020 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 hadi 24 ijayo.

Awamu zinazofuata zitajumuisha ujenzi wa miradi mingine ya hoteli, makazi na biashara za rejareja karibu na majengo makuu. Awamu ya 1 ya mradi huu inatarajiwa kukamilika ndani ya miaka 4 ijayo.

Wanunuzi watarajiwa wanaweza kutembelea tovuti hii : www.blueamberzanzibar.com

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na :

GENE REDELINGHUYS | Meneja wa Mawasiliano wa Blue Amber Zanzibar

gene@pennyroyalltd.com

Related Posts

Comments

Stay Connected

22,044FansLike
0FollowersFollow
0SubscribersSubscribe

Recent Stories